GREEN VOICES YALETA UKOMBOZI KWA WAKAZI WA UKEREWE.

Baada ya sintofahamu ya muda mrefu kwa wakazi wa Ukerewe mkoani Mwanza, hatimaye mbadala wa zao la kilimo cha mihogo wapatikana baada ya mradi  unaopambana na mabadiliko ya tabia Nchi wa Green Voices kuanzisha kilimo cha zao la viazi lishe ili kupambana na baada la njaa lililotishia Wilaya hiyo hivi karibuni.Baada ya sintofahamu ya muda mrefu kwa wakazi wa Ukerewe mkoani Mwanza, hatimaye mbadala wa zao la kilimo cha mihogo wapatikana baada ya mradi  unaopambana na mabadiliko ya tabia Nchi wa Green Voices kuanzisha kilimo cha zao la viazi lishe ili kupambana na baada  la njaa lililotishia Wilaya hiyo hivi karibuni.  

Leocadia Vedastus, mshiriki wa Green Voices Wilayani Ukerewe amesema kilimo hicho ni tofauti na kilimo cha viazi vya zamani kwani viazi lishe vinatumia muda mfupi katika kukomaa na pia vinahimili magonjwa licha ya kugundulika kuwa na virutubisho vingi vya vitamini “A”, virutubisho ambavyo ni muhimu kwa watoto na kwa wanafamilia kwa ujumla.Afisa Lishe wa Halmashauri ya Wilaya hiyo, BwanaIssa Mgengi anasema viazi hivyo ni salama kwa chakula, licha ya kuwa vinalinda mazingira kwa kuwa vinakua kwa kutambaa, jambo ambalo pia linasaidia kukabiliana na mabadiliko ya tabia Nchi kwa kuzuia mmomonyoko wa Ardhi, “ anasema Bwana Mgengi “.Naye Stella Willison anasema mradi huo umekuja kwa wakati muafaka, licha ya changamoto anayoiona ya upatikanaji wa soko la bidhaa watakazozizalisha kutoka katika zao hilo.Tayari zaidi ya Kaya 25 zimenufaika na mradi huo unaotarajiwa kuwanufaisha wanawake wengine katika wilaya hiyo.Mkuu wa Wilaya ya Ukerewe Bwana Joseph Mkirikiti anasema ni furaha kubwa kwa mradi huo kuanza katika wilaya hiyo, na hususani kwa kuanza na wanawake wenyewe kwani wanawake ndio wanaofanya kazi za shamba na ndio wenye mzigo mkubwa wa kulea na kutunza familia, na hivyo kutoa wito kwa wanawake kumiliki mradi huo na kuhakikisha unafika katika visiwa vyote 38 .  

http://voces.mujeresporafrica.es/wp-content/uploads/IMG-20160422-WA0191.jpg

Pamoja na changamoto nyingine Bwana Mkirikiti anataja changamoto kubwa zingine katika Wilaya ya Ukerewe kuwa ni pamoja na kukosekana kwa elimu ya uzazi wa mpango, na uharibifu wa miundo mbinu unaopelekea wanawake wajawazito kusafirishwa kwa pikipiki wakati wa kujifungua, changamoto inayotokana na madhara ya mabadiliko ya tabia Nchi.      

  Posted by: Tukuswiga Mwaisumbe at MONDAY, 02th May 2016