MRADI WA MAJIKO BANIFU WATUA KIJIJINI MAGOZA, MKURANGA.

 

Wakazi wa kijiji cha magoza kata ya kiparang’ata, wilaya ya mkuranga mkoani pwani wamehimizwa kuchukua hatua kukabiliana na mabadiliko ya tabia nchi ambayo yameendelea kuwaathiri hasa wanawake kijijini humo na nchini kwa ujumla.

Kwa
mujibu wa mkuu wa wilaya ya mkuranga mh abdallah kihato wanawake ni kundi
linaloathiriwa zaidi na mabadiliko ya tabia nchi kutokana mazingira ya kazi
zao.

 Mkuu wa wilaya ya Mkuranga Mh. Abdallah Kihato (aliyesimama) akiwahutubia wananchi wa kijiji cha magoza waliohudhuria uzinduzi wa mradi wa majiko banifu wa green voices.

 

Mh
kihato amewata wakina mama kijijini magoza kutumia fursa ya mradi wa green
voices uliopita kijijini hapo ukisisitiza matumizi ya majiko banifu ama majiko
sanifu ambayo ni rafiki wa mazingira yakipunguza matumizi makubwa ya ukataji
miti na badala yake kutumia kuni chache na hivyo kupunguza adha ya kusafiri
umbali mrefu kusaka kuni.

Akiongea
wakati wa uzinduzi wa mradi huo mratibu wa green voices nchini Tanzania
secelela balisidya amesema mradi huo umewekeza kwa wanawake ukiwa na lengo la
kupaza sauti za wanawake katika suala zima la kukabiliana na mabadiliko ya
tabia nchi.

 Bi Secelela Balisidya akitambulisha mradi wa majiko banifu wa green voices katika sherehe za uzinduzi.

 

Kwa upande wake mwanzilishi na msimamizi wa mradi huo wa kutumia majiko banifu bi Regina Kamuli amesema ameamua kutekeleza mradi huo sehemu za kijijini kwasababu wakazi wa maeneo hayo ndio wahanga wakubwa katika matumizi ya kuni na kutoa wito kwa wakazi hao kujenga tabia ya kupanda miti kwani majiko hayo ingawa yanatumia kuni chache lakini bado yanahusisha matumizi ya kuni na zoezi zima la ukataji miti.

 

 Bi Regina Kamuli(mbele) akiwa na wanawake wanaounda kikundi cha Motomoto kijijini Magoza, watakaonufaika na mradi wa majiko banifu wa Green voices.

Mradi
huu wa Majiko banifu ambayo hutumia udongo pamoja na kinyesi cha ngombe, mlenda
unaotokana na mti wa mtamba, sukari na chumvi katika utengenezaji umepokelewa
kwa mikono miwili na wanawake kijijini hapo na kusema mbali na kuwa mwokozi
katika shughuli zao za kila siku yakiwarahisishia katika utafutaji wa kuni na
hata kupunguza shughuli za ukataji miti hovyo, majiko hayo yataweza kuwasaidia
katika kuongeza kipato kama watapata soko na kuyauza na hivyo kuinua uchumi wao.

 

Baadhi ya majiko banifu yenye kutumia kuni chache tofauti na majiko mengine ya kuni. Majiko haya ni rafiki wa mazingira kwani hupunguza ukataji wa miti kwa kiasi kikubwa. 

PICHA:

 Wanawake wa kikundi cha motomoto wakipata mafunzo ya ujenzi wa majiko banifu kutoka kwa mtaalam.

 mwanzilishi na msimamizi wa mradi wa majiko banifu wa green voices, Regina Kamuli akiwa na majiko banifu.

 

Regina Kamuli akiwa pamoja na wanawake wa kikundi cha motomoto katika shughuli za ujenzi wa majiko banifu. 

 Mkuu wa mkoa wa Mkuranga Mh Abdallah  Kihato akipanda mti katika kuwahimiza wananchi wapande miti kwa wingi kila wanapoikata kwa matumizi yao ili kutunza mazingira. 

 

Waandishi wa habari wa Green voices (kutoka kushoto Siddy Mgumia, Tukuswiga Mwaisumbe, Secelela Balisidya, Judica Losai, Farida Hamis pamoja na msimamizi wa mradi wa majiko banifu kijijini Magoza, Regina Kamuli wakiwa katika picha ya pamoja na mkuu wa mkoa wa Mkuranga Mh. Abdallah Kihato. 

 

Posted by: Farida Hamis, May 19th, 2016.